Pakistan jijini Karachi, vyombo vya habari vimeripoti juu ya vifo vya watu 65 waliofariki dunia kutokana viwango vya juu vya joto lililoikumba mji huo katika siku tatu mfulilizo msimu huu wa mfungo wa ramadhani kwa waislamu.

Ambapo siku ya jumatau kulikuwa na nyuzi joto 44 hali ambayo iliwawia vigumu hasa waislamu ambao wamefunga kula chakula na kunywa maji kipindi cha siku.

Karibu miili 114 ilidhurika na joto kali jijini humo na kukimbizwa katika Taasisi ya kutoa misaada ya kijamii ya Edhi iliyopo Karachi, ambapo kati yao watu 65 walifariki dunia.

Hata hivyo matukio hayo ya vifo yanaaminika kutokea yakichochewa na kukatika kwa umeme katika jiji hilo huku sababu nyingine ikitajwa kuwa wagonjwa hao kuchelewa kupatiwa matibabu ya haraka.

Idadi kubwa ya watu waliofariki kwa kudhurika na joto kali walikuwa kutoka maeneo ya makazi ya Landhi na Korangi.

Taarifa zinaeleza kuwa wagonjwa wengi walifia majumbani kwao na idadi kubwa ya watu waliofariki ni wazee wenye umri wa miaka kuanzia 78.

Aidha hii si mara ya kwanza vifo vya aina hii kutokea jijini Karcahi, ambapo mnamo mwaka 2015  joto lilifika nyuzi joto 45 na kusababisha watu takribani 1300 kufariki dunia wengi wakiwa wazee na wagonjwa.

Joto linatabiriwa kubaki juu ya nyuzi joto 40 kwa siku chache zijazo na kushuka kidogo mwishoni mwa wiki.

EXCLUSIVE: Nimepata bahati kubwa sana, nilikuwa navizia wakati huo- Prof. Kitila Mkumbo
Video: Ni kweli kwamba nchi yetu ni masikini- Prof. Kitila Mkumbo