Watu zaidi ya milioni moja wamehifadhiwa katika kambi za muda ili kuepuka mafuriko ambayo yameua zaidi ya watu 410 katika jimbo la kusini magharibi mwa India la Kerala, huku zaidi ya nyumba 50,000 zikiharibiwa.

Waathirika hao wa mafuriko wanazidi kukimbilia katika makambi wakati kiwango cha uharibifu kikianza kuonekana kutokana na maji kuanza kupungua.

Aidha, Miili sita ilipatikana jana Jumatatu na kufanya jumla ya idadi ya watu waliofariki kufikia 410 tangu msimu wa masika ulipoanza mwezi Juni.

Timu za uokoaji za wanajeshi zimesema kuwa watu wamebaki katika makazi yao elfu kadhaa katika mji huo wamebaki katika nyumba zilizoharibiwa na mvua za siku kumi ambazo zimelikumba jimbo hilo.

Hata hivyo, vikosi vya uokoaji vya wanajeshi wa kitengo cha wanamaji na anga wamesambaa maeneo yote ya jimbo hilo ili kuwasaidia wale waliokwama katika maeneo ya ndani na milimani, huku helikopta na ndege zisizo na rubani zikifanya kazi ya kudondosha vyakula, madawa na maji katika vijiji ambako mawasiliano yamekatika.

Tuzo za MTV – VMAs: Orodha kamili ya washindi
Mashabiki 'wamzira' Kevin Hart kwa kumtusi Trump

Comments

comments