Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo kati ya Klabu ya Yanga na Town Rollers utakaochezwa hii leo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika taarifa iliyotolewa hii leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten imemtangaza Waziri Dkt. Mwakyembe kuwa ni mgeni rasmi.

Taarifa hiyo ya Dismas imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe ndiye ataongoza maelfu ya mashabiki wa soka nchini watakaojitokeza kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huo.

“Kwenye mchezo wa leo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC toka Botswa mgeni rasmi atakuwa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe,”imeeleza taarifa hiyo

Hata hivyo, Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10: 00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Taifa na baada ya wiki moja timu ya Yanga itasafiri kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mechi ya marudiano.

 

 

Waamuzi watanzania hatarini kufungiwa
Wachungaji 6 waswekwa ndani