Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujezi wa uwanja wa Uhuru maarufu shamba la bibi na kupitia maeneo mbalimbali ya Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Majaliwa aliambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye pamoja na katibu wa wizara hiyo Elisante Ole Gabriel.

Pamoja na ukaguzi huo Waziri mkuu Majaliwa alionyeshwa ramani ya uwanja wa Uhuru inayoonesha uhalisia pindi ukarabati wake utakapokamilika.

Mbali na ukaguzi huo Majaliwa alikutana na kuteta na viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo kwa lengo la kupokea changamoto zinazowakabili na kujadili maendeleo ya michezo nchini.

Kitaaluma Waziri mkuu, Majaliwa ni kocha wa mpira wa miguu ambapo kwa sasa ana cheti cha kozi ya leseni B ya ukocha, inayompa nafasi ya kufundisha klabu yoyote ya Ligi Kuu hapa nchini.

Mzazi Wa Cavani Ataka Mwanae Achezee Timu Hizi
Wema Sepetu atoa ya Moyoni kuhusu ujauzito wake