Msanii na mrembo maarufu Wema Abraham Sepetu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushambuliwa kwa maneno makali na baadhi ya mashabiki kufuatia moja ya post aliyoweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Hilo limetokea leo Januari 6, 2022. Muda mfupi tu, baada ya mrembo huyo kuweka tangazo la tiba lililoambatana na ushauri wa mambo kadhaa yanayopaswa kuzingatiwa na wanawake wenye kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Chapisho hilo liliendelea kutoa maelekezo ya jinsi ya kumpata mtu sahihi anayeweza kutoa msaada wa kitabibu kwa undani zaidi juu ya suala hilo.

Baadhi ya mashabiki waliokutana na post hiyo ya Wema wameonyesha kutoridhishwa na kitendo cha mrembo huyo kuweka tangazo hilo hasa likiambatana na picha inayomuonyesha mtoto mchanga akiwa mikononi mwa wahudumu wa afya wakati mzazi akifanyiwa upasuaji.

Wema Sepetu, mrembo aliyewahi kulishika taji la Miss Tanzania mwaka 2006, amekuwa akiutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutangaza biashara mbali mbali kama sehemu ya kujiingizia kipato licha ya changamoto kadhaa za namna hii kujitokeza.

Gwajima afunguka kuhusu kuongoza ‘Sukuma Gang’ kumkwamisha Rais
Tuzo za Grammy zaahirishwa