Mwezi mmoja baada aliyekua nahodha wa kikosi cha FC Barcelona, Xavi Hernandez kupishana maneno na Cristiano Ronaldo kwa kusema mshambuliaji huyo kutoka nchini Ureno hawezi kujilinganisha na Lionel Messi, mkongwe huyo amezungumzia nafasi ya mchezaji huyo wa Real Madrid kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

Xavi amesema kwa uwezo ambao anaonyesha kwa sasa Ronaldo anaamini staa huyo ana nafasi ya kushinda tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa mwaka huu.

“Cristiano ana nafasi kubwa ya  kushinda Ballon d’Or mwaka huu, ameshinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la Euro akiwa na Real Madrid na Ureno,

“Lakini nafikiri jambo hilo litakuwa na ushindani mkubwa, kwa sababu hata Messi yupo,” alisema Xavi.

Maadhimisho ya mtoto wa kike kitaifa kufanyika oktoba 11 mkoani shinyanga
Amissi Tambwe: Sina Uadui Na Simba Hata Kidogo