Meneja wa Man City Pep Guardiola, amejipanga kumtumia kiungo kutoka nchini Ivory Coast Yaya Toure katika nafasi ya beki wa kati, badala ya Vincent Kompany ambeya kwa sasa ni majeruhi.

Kompany alipata majeraha ya goti katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Crystal Palace na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa majuma saba yajayo.

Toure alianza kuonekana katika kikosi cha Man City kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu, kutokana matatizo yaliyoibuka baina ya wakala wake na Pep Gardiola.

Guardiola anajipanga kufanya mabadiliko ya kumtumia Toure katika nafasi ya ulinzi, kwa kigezo cha kuwahi kufanya hivyo walipokua FC Barcelona.

Sifa ya urefu na umakini wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, imechukuliwa kama kigezo kikubwa kwa Guardiola cha kutaka kutumia kama beki wa kati, jambo ambalo mpaka sasa halijaaminiwa vilivyo na mashabiki wa Man City.

Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako
GGM yapigwa faini ya milioni 10