Mgodi wa  dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM) umetozwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kosa la kutokuwa na huduma ya choo mgodini hapo, adhabu hiyo imetoleawa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.

Adhabu hiyo imekuja mara baada ya Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina Mkoani Geita.

Mpina ameuagiza uongozi wa mgodi huo kujenga miundombinu rafiki kwa mazingira yatakayopelekea maji hayo kwenda katika mkondo sahihi..

Kwa upande wa  mmoja wa wakazi wa kijiji cha Katoma, Magori James alisema kuwa vumbi na maji ya mvua vinavyotoka kwenye mgodi huo vimekuwa ni kero na changamoto ya muda mrefu katika kijiji hicho.

Pamoja na malalamiko ya wakazi wa Katoma Geita kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi huo pia umefanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambaza maji safi a salama katika mji wa Geita ukishirikiana na  mamlaka ya maji safi na taka katika Mkoa huo.

Yaya Toure Kupewa Mtihani Mpya Man City
Video: Magufuli awatia kitanzi Gavana, bosi wa TRA, Katibu wa Fedha, CUF wachapana mbele ya jaji...