Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wametamba kuisambaza US Monastir ya Tunisia, katika mchezo wa Mzunguuko watano wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa mchezo huo Jumapili (Machi 19) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo wakiendelea kuhamasika kufika uwanjani kuishangilia timu yao mwanzo mwisho.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa wanatambua kazi kubwa wanayo dhidi ya Waarabu hao wa Tunisia, lakini watawafanyia jambo la kipekee ambalo hawataamini.

“Tuliwafuata, wakatufunga unadhani kuna ambaye alipenda? Hakuna aliyefurahia matokeo yale sasa wanakuja Uwanja wa Mkapa kitakachowakuta hao Waarabu hawataamini kila kitu kinakwenda kwa mpangilio mkubwa na sasa wanakuja ili kutupa tiketi ya kutinga robo fainali Kombe la Shirikisho.”

“Mchezo wenye hadhi ya mchezo wa maamuzi na wachezaji wanatambua kwamba kila mmoja anahitaji ushindi, wajitokeze kwa wingi ili kushangilia na kutakuwa na aina tofauti ya ushangiliaji ili kuwapoteza wapinzani wetu,” amesema Kamwe.

Young Africans inasaka alama tatu ili kufikia malengo ya kutinga Hatua ya Robo Fainali, baada ya kujikusanyia alama 07 zilizotokana na ushindi dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo na AS Real Bamako ya Mali ambayo pia iliambulia sare ya katika uwanja wa nyumbani wa Machi 26, mjini Bamako.

Wanasiasa washauriwa kunadi sera si kutoa lawama
Ouattara aondolewa kikosini Simba SC