Baada ya kufanikiwa kufanya uchaguzi wake wa viongozi mwezi Juni mwaka huu na Mwenyekiti wake, Yusuf Manji kutetea nafasi yake, klabu ya Young Africans inatarajia kufanya mkutano mkuu wa Wanachama Agosti 6 mwaka huu katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay, Dar es salaam kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

Taarifa iliyotumwa na kaimu Katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema pia siku hiyo baada ya mkutano huo, Jioni Yanga watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mahakama imetangaza tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili Tundu Lissu. Mbunge Nasari aachiwa huru
Edgardo Bauza Akabidhiwa Mikoba Ya Gerardo Martino