Young Dar es Salaam amezungumzia uhusiano uliopo kati yake na rapa wa kike the Goddess Rosa Ree, baada ya kuenea kwa tetesi kuwa huenda wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi kutokana na ukaribu wao.

Akifunguka hivi karibuni kupitia The Playlist ya Times Fm, Young Dee alikanusha tetesi hizo, na kueleza kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rosa Ree, bali kinachowakutanisha ni muziki wao tu.

“Hatujawahi kudate mimi na Rosa Ree, tulikuwa washkaji tu. Ni kwa sababu yeye ni rapa na mimi ni rapa kwahiyo tunakutana kwa sababu ya kazi ya muziki… ni kama mimi na wewe kinachotukutanisha hapa ni hii kazi, hatuuzi vitumbua,” alijibu swali la Lil Ommy, mtangazaji wa The Playlist.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu maswali ya wengi kuwa huenda wawili hao walikuwa wapenzi lakini sasa wameachana, Young Dee alisema bado hawajaachana [kama washkaji], na kueleza chanzo cha ukaribu wao.

“No, hatujaachana. Kwa sababu ni mtu ambaye anafanya kazi zake na mimi nafanya kazi zangu. Kilichotukutanisha ni kwasababu watu wote ambao sisi tulikuwa tunafanya nao kazi walikuwa watu wa karibu,” alifunguka.

Katika hatua nyingine, rapa huyo ambaye ameachia audio na video ya ‘Naoa’, alikiri kuwa kuna wimbo amefanya na Rosa Ree, lakini kwakuwa bado ni mapema, mengi kuhusu mradi huo yatajulikana muda utakapofika.

Rosa Ree ni rapa wa kike ambaye kwa hivi sasa anaonekana kuongoza mashambulizi ya mistari na mitindo ya kughani, akishika vichwa vingi vya habari na kuwavuta wasanii wengine wakubwa kufanya naye kazi.

Hivi karibuni, Fid Q amemshirikisha kwenye ‘Ole Chizza’.

Video: Mitandao yamkamatisha Mmarekani aliyempiga vibao mhudumu
Tyson Fury na Wilder wavimbishiana misuli ulingoni