Mvulana wa miaka 17, Dylan Butler amemuua Mwanafunzi mmoja wa darasa la sita na kuwajeruhi wengine watano baada ya kuwafayatulia risasi wakati wakiwasili shuleni baada ya likizo ya majira ya baridi.

Mtuhumiwa huyo, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili ya Perry aliwafyatulia risasi wanafunzi wa shule ya Iowa na baadae alikutwa amekufa kutokana na jeraha la risasi.

Tukio hilo lililotokea siku ya kwanza ya kufungua shule huko Iwoa ni sehemu ya janga la kitaifa la machafuko ambayo yameongezeka ya kutumia silaha mashuleni.

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya kuchunguza uhalifu ya jimbo Mitch Mortvedt, amesema Butler alituma machapisho kadhaa mtandaoni kabla ya tukio hilo.

Coastal Union kurudi kambini, wawili wasajiliwa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 5, 2024