Mshambuliaji kinda Kylian Mbappe, ameripotiwa kukubali kujiunga na Real Madrid bure mwishoni mwa msimu huu 2023/24.

Mbappe amemaliza minong’ono mingi kuhusu hatima ya maisha yake baada ya kufichua kwamba atakwenda Bernabeu dirisha la majira ya kiangazi litapofunguliwa.

Mwandishi wa Foot Mercato, Santi Aouna amesema Mshambuliaji huyo mshindi wa Kombe la Dunia 2018, amefikia makubaliano ya kujiunga na miamba hiyo ya Hispania.

Aouna amesisitiza kwamba Mbappe mwenye umri wa miaka 25, atakuwa mchezaji wa Real Madrid msimu ujao.

Manchester United na hata Liverpool nazo zilihusishwa na mpango wa kumsajili Mshambuliaji huyo wa Ufaransa.

Inafahamika wazi Mbappe aligomea ofa tamu kabisa ya mkataba wa pesa nyingi huko Saudi Arabia.

Staa huyo anaingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake huko PSG, hiyo ina maana anaweza kuzungumza na klabu ya yoyote  juu ya uwezekano wa kusaini mkataba wa awali ili aondoke bure mwishoni mwa msimu, dili lake litakapofika ukomo.

Mbappe, aliyechezea Ufaransa mechi 75 na kufunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Argentina, anaweza kufanya uamuzi wa kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake PSG kama atahitaji kufanya hivyo.

Lakini mapema tu mwaka jana wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi aliwaambia mabosi wa miamba hiyo ya Ligue 1 kwamba, hana mpango wa kubaki hapo baada ya msimu huu kumalizika.

Ahmed Ally: Hatujapokea ofa yoyote
SMZ yapanga kuondoa zamu mbili za Wanafunzi