Mtanzania Prudencia Paul Kimiti ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Watoto wetu Tanzania kilichopo Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni nia yake ya kumshukuru Mungu kwa kupata tuzo ya kufanyakazi kwa bidii nchini aliyopewa Nchini Uingereza na Malkia Elizabeth.

Msaada huo uliotolewa ni wa vitu mbalimbali ikiwemo madaftari, sukali, mikeka ya kukalia, biscuit, pipi, pampas za watoto, juisi, taulo za kike, miswaki, pesa za nunua mtungi mkubwa wa gasi na mafuta ya kupikia.

“Mwenyezi Mungu akasaidia mwaka jana nilipata bahati ya kupewa tuzo na marikia Elizabeth wa uingereza kabla hajafariki hivyo nimeona nije kutoa msaada huu ikiwa ni kumshukuru Mungu,” alisema Prudensia.

Aidha, amesema tuzo hiyo aliyopewa sio ya pongezi kwaajili yake pekee bali ni pongezi kwa watanzania wote na pongezi kwa taifa zima la Tanzania, huku akiwataka watoto hao wa kituo cha Watoto wetu Tanzania, waishi vizuri kwa kupendana, wasaidiane kwani wote ni ndugu

“Hata ukimuona mwenzako anapata shida yoyote hata kwenye masomo umsaidie kwani watoto wote katika kituo hicho ni ndugu kwahiyo naombeni sana mpendane na kusaidiana,” alisema.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 22, 2024
Dkt. Biteko, Waziri wa Nishati Misri wajadili Mradi JNHPP