Ushirikiano uliopo, kati ya Tanzania na Korea Kusini umechochea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo mradi wa kimkakati wa daraja la Tanzanite, lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini kupitia mfuko wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi (Economic Development Cooperation Fund -EDCF)

Hayo hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano yaliyohusisha Ofisi ya Waziri Mkuu na National Agency for Adminstrative City Constraction and Heerim Architects and Planners ya Nchini Korea Kusini.

Amesema, “kupitia kusainiwa kwa hati hizo Tanzania itanufaika na teknolojia ya kisasa ya usanifu na ujenzi wa majengo na miundombinu mingine itayopendezesha Mji mkuu Dodoma, sambamba na kupatikana kwa fursa mpya za ushirikiano na makampuni ambayo yana uzoefu mkubwa wa usanifu na ujenzi hususani wa majengo katika miji na majiji makubwa.”

Hata hivyo, Mhagama amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alivyokuwa Korea Kusini aliitembelea taasisi ya National Agency for Administrative City Construction, ambayo ni wakala wa kitaifa Nchini humo wanaosimamia na kuendeleza ujenzi wa Jiji la Sejong nchini humo, lililojengwa kwa mandhari nzuri.

Ameongeza kuwa, muonekano wake wa kuvutia ulimfanya Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa taasisi hii Nchini Tanzania ili kubadilishana uzoefu na viongozi wa taasisi zinazofanana na hizi za hapa Nchini Tanzania.

TANESCO ifanye ukaguzi mara kwa mara vituo vya umeme - Dkt. Biteko
PAC yaishauri Serikali kufanya kazi na OSHA