Rais wa Senegal Macky Sall, ameapa kuandaa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo baada ya Baraza kuu la kikatiba kubatilisha uamuzi wa kuchelewesha uchaguzi.

Jana (Februari 16, 2024), Baraza la Katiba la Senegal, lilibatilisha tangazo la kuchelewesha uchaguzi wa rais, uliokuwa ufanyike mwezi huu likisema kura ya Bunge ilikuwa kinyume na katiba likidai muswada uliopitishwa ulikuwa kinyume na katiba.

Hivyo, Ofisi ya rais imesema Rais Sall anakusudia kutekeleza kikamilifu uamuzi wa Baraza Kuu la Kikatiba na kwamba atafanya mashauriano muhimu ya kuandaa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo.

Uamuzi wa Rais Sall wa kuchelewesha uchaguzi wa Februari 25, umeitumbukiza Senegal katika mzozo mbaya wa kisiasa, baada ya kutokea kwa machafuko yaliyotokana na maandamano makubwa ya raia na vyama vya upinzani.

Mfumo ufundishaji mubashara umefika kwa wakati - LAAC
Lowassa alikuwa mchapa kazi hodari - Dkt. Nchimbi