Wafuasi tisa wa Chama cha ANC cha Afrika ya Kusini  wamefariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye mkutano wa kampeni kupata ajali karibu na mji wa Paulpietersbug.

Taarifa ya Mamlaka ya Usalama Barabarani nchini humo, imeeleza kuwa basi hilo lilipata ajali baada ya kupoteza mwelekeo, likiwa na watu 70 na baadhi yao walijeruhiwa.

Watu wanane walikufa papo hapo na mmoja alifariki baadaye baada ya kufikishwa hospitalini.

Waliopata ajali ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa wamehudhuria katika uwanja wa mpira jijini Durban siku ya Jumamosi Februari 24, 2024 katika uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya ANC.

Afrika Kusini inatarajia kufanya uchaguzi wa kitaifa na majimbo Mei 29, 2024.

Ajali iliyoua 25: Sajini atoa maelekezo kwa Polisi
Picha: Matukio ya ajali iliyouwa 25 Arusha