Watu tisa wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria aina ya Noah lenye namba za usajiri T795 BIS kusombwa na maji kwenye mto Kisimani katika Kijiji cha Lumeme kilichopo Halmashauri ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akithibirisha kutoka kwa tulio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea Machi 11, 2024 baada ya gari hilo kusombwa na maji.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva ambaye alilazimisha kuvuka wakati Mto huo ukiwa umejaa maji, huku akitoa rai kwa Madereva na Wananchi kuacha tabia ya kupima maji katika madaraja kwa kuyatazama.

Amewataja waliofariki kuwa ni Edwini Abeli Ngowoko (55), Matengo (Dereva wa Gari), Valeliana Ndunguru (18), Innocent Cassian Ndunguru ( 63), Simon Mahai (21) na Nathan Kumburu (39)”

“Wengine ni Faraja Daud Tegete (18) ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kilumba, Ebiati Daud Tegete (2) na Alfonsia Casian Mbele (40).

Wenye nia njema, ovu watembelee Makaburi ya Kimbari
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 13, 2024