Mastaa wa Manchester United wameripotiwa kufungua milango kwa mchezaji mwenzao, Mason Greenwood kurudi kuichezea timu hiyo ya Old Trafford.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alikuwa na hofu huenda maisha yake ya kuichezea Man United yamefika mwisho baada ya kutolewa kwa mkopo huko Getafe ya Hispania, kutokana na sakata lake la kesi ya kubaka.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa na Greenwood alionekana hana hatia, lakini shida ilikuwa kwenye kupata nafasi ya kuichezea Man United na mapingamizi yalikuwa mengi.

Tajiri mpya wa Man United, Bilionea Sir Jim Ratcliffe alisema milango ipo wazi kwa mshambuliaji huyo kurudi Old Trafford, baada ya msimu huu kuonyesha ubora mkubwa akiwa amefunga mabao manane na kuasisti matano kwenye La Liga akiwa na kikosi cha Getafe.

Sasa, ripoti zinadai wachezaji wa Man United wanapiga kura mwenzao arudi.

Chanzo kilifichua: Wachezaji wenzake wala hawapingi kuhusu kurudi Old Trafford.

Wanafahamu kila kitu na ukweli wa kile kilichokuwa kinamkabili, hivyo wanamtaka arudi. Uamuzi wao umelenga kwenye soka.

“Man United inapata shida kufunga mabao, hivyo inahitaji mtu kama Mason. Wanamtazama akifunga na kutengeneza mabao huko Getafe kila juma.”

Mkataba wake kwenye kikosi cha Man United utafika tamati 2025.

Na hivi karibuni, kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alisema milango ya staa huyo kurudi kwenye timu ya taifa ipo wazi.

Kikosi cha timu ya soka ya wanawake ya Man United ndicho kinachoonekana kupinga Greenwood kurudi.

Kopunovic yupo kikaangoni Tabora Utd
Benchikha afunguka kambi ya Zanzibar