Mfumo wa Unununuzi wa Mazao kwa njia ya Mtandao unaoedeshwa na Soko la Bidhaa Tanzania – TMX, umeongeza ushuru wa mapato mkoani Kagera kwa zaidi ya asilimia 200 ambapo kwa misimu miwili Serikali kupitia TMX, imeanza utekelezaji wa ununuzi wa Bidhaa kwa zao la Kahawa mkoani humo, ili kuongeza tija katika kilimo.
Akizungumza mjini humo, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Uchumi wa Mkoa wa Kagera, Isaya Tendega alisema kabla ya mfumo huo Manisapaa ilikuwa ikikusanya ushuru wa Shilingi 1. 2 bilioni kwa mwaka na kuongeza kuwa umepunguza malalamiko kwa Wakulima na kurahisisha ukusanyaji wa ushuru.
Amesema, kazi ya kukusanya ushuru sasa imekuwa rahisi bila kukikimbizana kwa kuwa kila kitu kipo katika mfumo, huku Afisa Mipango wa TMX, Eva Msangi akidai kuwa mpango huo wa manunuzi katika zao la Kahawa umetekelezwa kuanzia msimu wa mwaka 2022/2023 na 2023/2004.
Hata hivyo, amesema tathimini inaonyesha kuwa Wakulima na Wanunuzi wanaufurahia mfumo huo kwani umerahisisha kupata fedha zao kwa wakati ambapo mwaka 2018/2019 ulikuwa na changamoto kubwa ya soko la Kahawa jambo lililochangia bei kuporomoka kwa kasi, huku Wakulima wengine wakiamua kung’oa miche ya Kahawa na kupanda ndizi pekee.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 22, 2024
Fahamu mambo 10 kuhusu mauaji ya kibaguzi Soweto