Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Sheria na Mawakili wa Serikali nchini kutekeleza majukumu kwa kuzingatia weledi, usawa na uadilifu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki bila kujali hali zao za kiuchumi.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akifugua mkutano wa Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Amesema, Serikali kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi wote, imeendelea kuchukua hatua kadhaa zikiwemo ujenzi wa miundombinu, uendelezaji wa rasilimali watu, maboresho ya mifumo na sheria mahsusi.

katika hatua nyingine, Majaliwa amesema Serikali imetekeleza mpango wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, Vituo sita Jumuishi vya Utoaji Haki, Mahakama za Wilaya 27 pamoja na mahakama za mwanzo 14, pia inaendelea na ujenzi wa vituo jumuishi sita vya Geita, Simiyu, Njombe, Katavi, Songea na Songwe.

Jaji Mkuu: Sheria zitatumika vyema kutoa haki
CHAN 2024 yanukia Afrika Mashariki