Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern Munich, Max Eberl, amesema klabu hiyo imetoa ofa ya mwisho kwa mlinzi wa kushoto wa Canada, Alphonso Davies, ili kuongeza mkataba wake huku kukiwa na taarifa za kutakiwa Real Madrid.

Mkataba wa Davies na Bayern unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, kumaanisha klabu hiyo ya Bavaria inaweza kumpoteza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ifikapo mwakani kwa uhamisho wa bure.

Ripoti za vyombo vya habari vya Hispania zinasema, Davies tayari amefikia makubaliano na Real Madrid kuhusu uhamisho huo, lakini Eberl alisema viongozi hao wa La Liga hawajawasiliana nao.

“Naweza kusema tulimpa Alphonso ofa thabiti na ya shukrani. Wakati fulani maishani lazima useme ndio au hapana,” alisema Eberl akiliambia jarida la Sport Bild

Bayern Munich bado wanaweza kuamuru ada ya uhamisho ikiwa Davies ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

“Hakuna klabu inayotaka kupoteza wachezaji bure,” alisema Eberl

Vyanzo vimeiamnbia ESPN wakati Madrid wakiendelea kumtaka Davies, hawako tayari kulipa zaidi ya euro milioni 40 ili kumsajili msimu huu wa joto na wako tayari kungoja mwaka mwingine kupata huduma yake kwa uhamisho wa bure.

Nia ya Davies ni kujiunga na Madrid, vyanzo viliongeza Davies, ambaye amefunga mabao 15 katika mechi 45 alizoichezea Canada, amecheza mechi 127 za Bundesliga akiwa na Bayern.

Davies ambaye ni raia wa Canada aliyezaliwa nchini Ghana, alijiunga na Bayern Januari mwaka, 2019 baada ya klabu hiyo kukubaliana uhamisho wa dola milioni 22 na Vancouver Whitecaps mwaka mmoja kabla ya mchezaji huyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 17.

Uwanja wa Mkapa kaa la moto kwa waarabu
DEEP Challenge Fund kuboresha mkakati athari za umasikini