Mfuko wa DEEP Challenge Fund Tanzania, umelenga kuboresha mkakati wa kitaifa, sera, na programu zinazoathiri umaskini na mazingira magumu ya umaskini nchini Tanzania, kwa kufadhili watafiti na wachambuzi wa kitaifa ili kutoa maarifa na ushahidi unaoendana na mahitaji ya watunga sera.

Hayo yamebainishwa hii leo Machi 22, 2024 na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Sera ya Oxford Ofisi ya Tanzania na Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya DEEP, Dkt. Charles Sokile katika Shule ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuongeaza kuwa ufadhili mpya wa fedha za utafiti pia unalenga kukabiliana na umaskini nchini kwa kufadhili utafiti wa ndani unaokidhi mahitaji ya watunga sera wa kitaifa.

Amesema, “ni wakati wa kusisimua nchini Tanzania, mpango mkakati wa maendeleo ya Dira ya 2050 ni fursa ya mara moja kwa kizazi kuunda mustakabali wa nchi yetu. Na kwa hivyo, data na uthibitisho kuhusu njia bora zaidi na za kudumu za kuweza kukabiliana na umaskini zitakuwa na jukumu muhimu katika kuunda dira ya nchi.”

Dkt. Sokile ameongeza kuwa, DEEP Challenge Fund ulilenga Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutokana na changamoto zake kubwa za kupunguza umaskini, tamanio na hitaji la ushahidi wa kitafiti na mabadiliko ya sera. Mfuko huu utaanza kutumika nchini Bangladesh na Nigeria baadaye mwaka huu. Mtazamo wa utafiti, malengo na upeo wa Mfuko wa Changamoto Tanzania unaundwa na watunga sera wa Tanzania na wadau wengine wakuu.

Katika uzinduzi huo, wahudhuriaji wa warsha wamejifunza kuhusu data na ushahidi unaohitajika ili kusaidia watunga sera kukabiliana na umaskini nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na vipaumbele vya utafiti na ushahidi wa pengo la kiutafiti vilivyoainishwa na kazi mpya za DEEP, itakayosaidia waombaji kukuza mawazo na uchanganuzi ambayo ni muhimu kwa sera na programu za kitaifa au Dira inayoibuka ya 2050.

Aidha, Maombi ya ufadhili wa mfuko huu yatafunguliwa baada ya kufanyika kwa warsha. Ufadhili mdogo na wa kati utatolewa kwa mashirika na/au watu binafsi kufuatia mchakato wa ushindani wa zabuni, huku mapendekezo ya kiutafiti yanayohimizwa ni yale ambayo yatasaidia kutoa maarifa mapya kuhusu vichochezi vya umaskini.

Vichocheo hivyo, ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi, UVIKO, ukuaji wa miji, uhamiaji, migogoro, Unyanyapaa wa jamii, na desturi za kijamii – au uchambuzi juu ya ‘nini kinafaa?’ kuhusiana na sera za serikali na programu zinazojumuisha malengo ya kupunguza umaskini.

 

Bayern Munich kutupa karata ya mwisho
Wachezaji Young Africans wamshangaza Gamondi