Watekelezaji wa mradi wa kuwezesha Wanawake na jamii kudai haki zao za Kidemokrasia na uongozi (SWIL), ZAFELA, PEGAO na TAMWA – ZNZ wametoa shuurani kwa wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi za kiserikali, Kijamii, Jamii, Waandishi Wahabari, Wahamasishaji jamii, Viongozi wa Dini na Taasisi binafsi, kwa kushiriki utekelezaji wa mradi ulioanza utekelezaji wake mwaka 2020 hadi na kumalizika kwake 2023.

Shukrani hizo, zimetolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) TAMWA – ZNZ na kuwasilishwa na Mkurugenzi wa TAMWA – ZNZ, Dkt. Mzuri Issa.

Ameeleza kuwa, kupitia mikutano ya kijamii tumeweza kufikia jumla ya jumla ya watu11, 129wengi wakiwa ni wanawake katika mikoa yote ya Zanzibar kupitia mikutanoyauhamasishaji, majadiliano, ufuatiliaji na mafunzo mbali mbali ambapo mradi umewawezesha wanawake 200 waliojengewa uwezo kuhusu masuala ya kidemokrasia, siasa na uongozi, ili waweze kushiriki katikavyombo vya maamuzi.

Aidha, taarifa hiyo imesema, jumla ya Waandishi wa Habari 199, wamejengewa uwezo wakuandikahabari zinazogusa masuala muhimu kuhusu haki za wanawake najamii,ambapo jumla ya habari 2,127 ziliandikwa kupitia radio, magazeti na mitandaoya kijamii na kuibua mijadala na kuchochea uwajibikaji wa taasisi mbalimbal, ambazo zilisaidia kuleta matokeo chanya katika jamii.

“Tumepitia sheria mbali mbali pamoja na Sheria ya Kadhi 2017, Sheriayautumishi wa umma (kushiriki katika siasa) No.03 2003, Sheria ya BarazalaVijana No.16 2013, Sheria ya uchaguzi No. 4 2018, sera ya jinsia yaTumeyaUchaguzi, Sheria ya utumishi wa umma 2011, Sheria ya vyama vya siasaCAP258 2002 na Sheria ya Tawala za Mikoa cha No.7 2014,” ilieleza taarifa hiyo.

Dkt. Mzuri alieleza kuwa, waliweza kukutana na wahusika mbali mbali wakiwemo Serikali, viongozi wadini, viongozi wa vyombo vya habari ili kuomba mabadilko ya sera, miongozo, utendaji na uwajibikaji ambapo mradi huo ulilenga kumuwezesha Mwanamke ambapo ili siyo tu awe kiongozi bali kiongozi bora.

“Kwa hivyo, tuliweza kuwasimamia ili wawezekufikialengo hilo ikiwemo pia kuwafundisha sera na haki zao na kuweza kufuatiliahaki zao binafsi na haki za wanajamii. Hii tuliifanya kupitia Wahamasishaji jamii (CBs), ambao walijengewa uwezo katika masuala ya uongozi, siasanaKwa hivyo, waliweza kuibua changamoto zaidi ya 1,000 za jamii nazamtummoja mmoja. Zaidi ya changamoto 771 wameweza kuzichukulia hatua na zaidi ya 400 zimeshapatiwa ufumbuzi,” alisema.

Aidha, Waandishi wa habari kwa upande wao waliibua viongozi mbali mbali, waliibua maswali mbali mbali akitolea mfano habari kuhusu Ali Juma wa Meli NNe SACCOSS, alivyoanzisha na kuipaisha SACCOSS hiyo hadi kuwa na magari yake wenyewe na kutoa mkopo hadi milioni 10.

Ameongeza kuwa, Mwandishi Khadija Kombo aliandika habari kuhusu muwekekezaji aliyewekaukuta Michamvi ambapo watu walishindwa kupita na jitihada za wananchi kumkataza ziligonga mwamba. Baada ya kipindi chake kulichotokakwenyetelevisheni Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja aliingia kati na kumshauri muwekezaji huyo kuvunja ukuta huo.

“Tumendaa pia sera na madawati ya kijinsia na taarifa katika vyombo vya habari 11 ambavyo hadi sasa vyombo saba vimeshapitisha sera zake. Tumeaandaa tunzo za umahiri kwa Waandishi wa Habari na tumekuwa tukipata washindi. Jumla ya washindi 35 walipatikana na kati yao Wanawake ni 29 na wanaume 6. Tunatoa Pongezi za dhati kwa Mamlaka za uteuzi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutambua mchango wa Wanawake katika kuleta maendeleo, hivyo kuongeza idadi ya viongozi Wanawake katika kipindi chake uongozi,” alieleza Dkt. Mzuri.

Aidha, katika vyama amesema wameona mashirikiano na vyama vya siasa, CCM, chamachaACT kimeandaa sera ya kijinsia na hivyo kuwa na malengo ya kuletausawawa kijinsia katika chama. Hata hivyo, mradi ulikumbana na changamoto kadhaa, ikiwa ni pamojanaupatikanaji mdogo wa takwimu za nafasi za wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi, kukosekana kwa sera na sheria zinazolazimishausawawa kijinsia katika sekta zote, baadhi ya viongozi hawazingatii usawawakijinsia katika teuzi mbalimbali wanazozifanya pamoja na kukosekanakwasera ya jinsia katika vyama vya siasa.

“Vilevile, mifumo ya upatikanaji wa haki saa nyengine inakuwa ni kikwazokwawananchi kupata huduma kwa urahisi. Kwa mfano wale ambao hawanavyeti vya kuzaliwa Pemba. Kubwa pia ni ukosefu wa kanzi data za wanawake na uongozi kaitkangazi zote kwa mfano viongozi wa Bodi, wajumbe taasisi binafsi, na databaseyawanawake wanaoweza kuwa viongozi,” alifafaua zaidi.

Aliongeza kuwa, “Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi, tumejifunza umuhimu wakutumiavyombo vya habari katika kupaza sauti za jamii katika kuibua changamotozaona kuongeza uwajibikaji wa viongozi, muamko wa elimu kwa wanawakekuhusu haki zao umeonyesha kuwa unawezesha kudai na kufuatiliahaki zaona Ushirikiano na wadau mbalimbali umethibitisha kuwa muhimukatikakufanikisha malengo ya kijamii.”

Hata hivyo, kwa kuzingatia waliyojifunza na mafanikio yaliyopatikana, wamependekeza kuanzishwa kwa kanzidata ya viongozi wanawake waliyoko katika sekta mbalimbali, kuwepo kwa sera na sheria zinazolazimisha usawa wa kijinsia katika sekta zote na mifumo rafiki ya upatikanaji wa huduma za kijamii kwawananchi.

Vilevile wametoa shukurani kwa Ubalozi wa Norway nchini kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huo, na kutoa wito kwa wadau wote wa maendeleo kushirikiana katika kuwawezesha Wanawake na Jamii kwa ujumla, kudai haki zao za Kidemokrasia, Siasa na Uongozi.

Robinho ahukumiwa miaka tisa
Uwanja wa Mkapa kaa la moto kwa waarabu