Kutokana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA, imesema watumishi wa bandari hiyo watachagua endapo watabakia TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World.

Taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya TPA,  imeelekeza kuwa Watumishi watakaoridhia kujiunga na DP World kwa hiari yao, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao katika makao makuu ya TPA kabla au ifikapo Machi 29, 2024.

Aidha, kwa watumishi ambao hawatopenda kujiunga na DP World, wao watabaki TPA kwani mamlaka hiyo itaendelea kuhitaji watumishi watakaotoa huduma katika Bandari zake zinazoendelea kuboreshwa Nchini.

Balozi Dkt. Nchimbi: Pemba Saluti kwenu
Mataifa yalaani shambulio la Urusi, vifo vyafikia 115