Klabu ya Manchester United imewekeza nguvu kubwa zaidi kwenye mchakato wa kuipata saini ya winga wa Crystal Palace na Ufaransa, Michael Olise, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Awali, Man United ilikuwa ikitaka kumsajili mshambuliaji wa PSV, Johan Bakayoko, lakini inaonekana kuna vita kubwa kutoka kwa Liverpool na Manchester City’ ambazo pia zinataka huduma yake.

Mashetani Wekundu wameamua kukomaa na Olise mwenye umri wa miaka 22, kwa sababu wanaona hakuna ushindani mkubwa ikilinganishwa na Bakayoko.

Timu nyingi kutoka England zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Bakayoko kutokana na kiwango alichoonyesha tangu ajiunge na PSV, hususani msimu huu ambapo amefunga mabao manane na kutoa asisti 12 kwenye mechi 40 za michuano yote.

Kwa upande wa Olise alianza kuvutia vigogo kutokana na kiwango alichoonyesha kwenye michuano ya vijana ya Euro mwaka jana. Mkataba wa sasa wa Olise ambaye msimu huu amecheza mechi 11, unatarajiwa kumalizika 2027.

Kibadeni amkataa Manula dhidi ya Al Ahly
BMH kushirikiana na Lumumba huduma za kibingwa