Jeshi la Polisi Nchini limesema tayari limeimarisha ulinzi na usalama katika kuelekea Sikukuu ya Pasaka Machi 31,2024 ambapo Waumini wa Dini za Kikristo wataungana na wenzao Duniani katika kusherehekea siku hiyo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu kamishna wa Polisi, David Misime amesema Sherehe hiyo hutanguliwa na waumini wa dini hizo hukusanyika kwa wingi na kushiriki Ibada, ambazo hufanyika nyakati za mchana na usiku, siku za Alhamis, Ijumaa, Jumamosi, Jumapili na Jumatatu ya Pasaka.

Amesema, Jeshi la Polisi limeendelea kujiimarisha ulinzi na kuhakikisha kwamba ibada na sherehe hizo zinafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama wa kutosha ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kufanya doria katika mitaa na barabara zote kuu ili kuzuia uhalifu au uvunjifu wowote ule wa amani.

Misime ameongeza kuwa, katika barabara zote kuu, kutakuwa na doria za Askari ili kuzuia ajali za barabarani, Pamoja na kukagua watakao kiuka sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wakiwa wamelewa pombe na kujaza abiria kupita kupita kiasi.

Aidha, ametoa wito kwa Viongozi wa nyumba za ibada ambao watakuwa na ibada katika kipindi hiki cha Juma Kuu wasisite kuwasiliana na Viongozi wa Polisi katika maeneo yao ili washirikiane katika kuimarisha
usalama kwa kipindi chote.

Balozi Kingu ataka hamasa ufikiwaji wa Umeme
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 28, 2024