Idara ya usalama ya Urusi – FSB, inawashikilia washukiwa waliotoa ufadhili kwa watu walioshambulia ukumbi wa tamasha wa Crocus Kaskazini-Magharibi mwa Moscow zaidi ya wiki moja iliyopita.

FSB imesema washukiwa hao ni raia wanne wa kigeni, ambao walihusika  kuwapa vifaa magaidi na wamezuiliwa mjini Dagestan katika eneo la Caucasus ya Kaskazini nchini humo.

Video iliyotolewa na FSB ilionesha mwanamume ambaye hakutambulishwa akisema aliwapa silaha wahalifu hao kwenye mji mkuu wa Dagestani, Makhachkala.

Kundi la wanamgambo la dola la kiislamu IS, lilidai kuhusika katika shambulizi hilo la Machi 22, 2024 lililouwa watu 144 huku zaidi ya 550 wakijeruhiwa na baadhi wakiwa bado hawajulikani walipo.

Simba SC kuifuata Al Ahly kesho
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 2, 2024