Klabu ya Liverpool ipo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Beki wa Kulia Trent Alexander-Arnold ili kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi beki huyu wa kulia anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu na Jurgen Klopp pia ataondoka.

Trent ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwakani, amekuwa akihusishwa na Real Madrid ambayo inamuhitaji ili akaboreshe eneo lao la ulinzi linaloonekana kuwa na mapungufu.

Liverpool inataka kutumia gharama yoyote ili kumbakisha kutokana na umuhimu wake kwenye timu na katika kumshawishi iliamua hadi ukapteni.

Hata hivyo, ikiwa mazungumzo yatafeli Liverpool haitokuwa na budi zaidi ya kumuuza mwisho wa msimu huu, kwani ifikapo mwakani mkataba wake utakuwa unaenda ukingoni, hivyo itatakiwa kumuuza kwa bei ya hasara ama ishuhudie akiondoka bure.

Tangu kyanza kwa msimu huu 2023/24, fundi huyu wa kimataifa wa England amecheza mechi 29 za michuano yote.

Watanzania wamuenzi Sokoine kwa kufanya kazi: Dkt. B iteko
Mtemi Ramadhani: Viongozi Simba wafanye usajili wa maana