Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli akiwa Turiani Mkoani Morogoro katika Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyokwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Afya Yangu Haki Yangu,” amewataka Wananchi kuwa na desturi ya kupima afya mara kwa mara.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Nguli amesema Watu wengi wanadhani afya njema ni kuwa mnene, muonekano mzuri, afya njema na kutoumwa, lakini si kweli kwani dhana ya afya ni pana na mtu anaweza kuwa vyote hivyo lakini akawa ni mgonjwa.

Amesema, “pale mtu inapofika hatua anaanguka chini na anakata roho ndipo unafikiri huyu kalogwa, katupiwa jini, unampeleka kwa mganga wa Kienyeji kumbe huyo alikuwa na Presha, hakuwa akijijua alikuwa anajiona yuko sawa hivyo ni muhimu tupime afya zetu.”

Akimwakilisha Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Tumaini Haonga, Simon Nzilibili amesema takkriban Wananchi 92,561 wamefikiwa na huduma mbalimbali za afya.

Naye Mratibu wa Maadhimisho hayo Kitaifa, Grace Msemwa amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhakikisha jamii inapata elimu kwa usahihi kuhusu masuala mbalimbali pamoja na huduma za afya.

Mtemi Ramadhani: Viongozi Simba wafanye usajili wa maana
'Nichukue Bwana' yauwa watano, wawili mahututi