Eva Godwin – Dodoma.

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan  ataliongoza Taifa katika siku maalum ya maombi na dua kwa Taifa, itakayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Aprili 22, 2024.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu Kassim, Majaliwa wakati wa Uzinduzi wa Nembo na Kauli mbiu ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ambapo amesema Viongozi wa Kitaifa wa Dini zote watahudhuria katika ibada hiyo huku akitoa rai kwa viongozi wa Wilaya zote Nchini kusimamia na kuratibu Wananchi watakao hudhuria maombi hayo.

Amesema, “ nisisitize kila Mkuu wa Wilaya aanze kufanya uratibu ili nchi yetu yote ishiriki katika maombi na dua hizo.Viongozi wa Kitaifa wa Dini zote watahudhuria katika ibada hiyo, Aidha, wilaya zote hapa nchini zitaandaa maombi kwa Taifa yatakayofanyika katika siku hiyo”,amesema

Naye Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano zitazinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi Aprili 14, 2024 katika Uwanja wa Maisara, Zanzibar.

Amesema, “tukio hlo litatanguliwa na uzinduzi wa miradi ya maendeleo Viongozi Wakuu wa Kitaifa pamoja na Viongozi wengine wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo tukio la kwanza ni uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Muungano kitakachozinduliwa tarehe 23 Aprili, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam,” amesema.

Amesema, tukio la pili ni kutunuku Nishani za heshima kwa Viongozi mbalimbali Serikalini na Jeshini pamoja na Askari kwa kutambua mchango wao katika kudumisha Muungano wetu. Nishani hizi atazitunuku Mheshimiwa Rais tarehe 24 Aprili, 2024 katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Kauli mbiu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni “MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,’ TUMESHIKAMANA NA TUMEIMARIKA, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU’’.

Wajipanga kuhamasisha vita dhidi ya Rushwa, Malaria
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 9, 2024