Kiungo kutoka nchini Afrika Kuisni Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’amefichua siri ya Kiungo mwenzake wa Young Africans Stephen Aziz Ki anayetajwa kuwindwa na Mabingwa wa Soka Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ‘Masandawana’.

Aziz Ki anatajwa kuwatamanisha Mashabiki wa soka wa klabu hiyo ya mjini Pretoria, kufuatia kiwango kikubwa alichokionesha wakati wa michezo miwili ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Skudu ambaye ni raia wa Afrika Kusini amesema Aziz Ki amemwambia hafikirii kwenda kucheza soka katika ligi ya PSL, kutokana na Ligi hiyo kukosa ushindani kama ilivyo ile ya Tanzania Bara.

“Kwa kiasi fulani nilifanya mazungumzo na Aziz Ki, alitaja kiwango cha Ligi Kuu ya Afrika Kusini ‘PSL’ kwa sasa kimeshuka, anasema kimepungua kiwango, sijui ni kwanini ingawa, sikuweza kujibu [kwa] hilo ingawa, nadhani takwimu zinaweza kujieleza, ulinganisho unapaswa kufanywa sasa hivi kulinganisha na zamani.”

“Soka la Tanzania, kuna vilabu viwili ambavyo vilikuwa vinashiriki robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF, kupitia yanasemwa mengi kuhusu soka la Tanzania na sifa zinapaswa kutolewa kwao na TFF kwa kazi nzuri wanayoifanya,”

“Kuhusu huku Afrika Kusini, nadhani watu wapo katika hali ya kuridhika, wako sawa, wanachofanya vilabu vingi ni kucheza ili kuepuka kushuka daraja, Wachezaji wengi wanaona ni sawa tu kuchezea klabu ambayo inapambana tu kukwepa kushuka daraja, hawana matamanio ya kuhama na kushindana na Al Ahly, CR Belouizdad, timu zote za Kiafrika huko nje.”

“(Aziz Ki) Nadhani akilini mwake, anafikiria matamanio. Ndiyo, kuna pesa katika ligi ya PSL ni kitu unachotaka kuangalia, lakini pia unataka kujipa changamoto na kujikuza thamani na kiwango kwa hivyo nadhani hapo ndipo inapokuja. Labda ukiitazama kwa mtazamo wa ushindani, haitawezekanai.”

Hatma zuio la urais wa Zuma kutolewa leo
Wajipanga kuhamasisha vita dhidi ya Rushwa, Malaria