Johansen Buberwa – Kagera.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa – TAKUKURU, Mkoa wa Kagera imebaini upungufu wa asilimia 98.87 ya utekelezaji wa miradi 21, ikilinganishwa na kipindi kilichopita cha Oktoba hadi Disemba iliyokuwa asilimia 68.50 wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 24 kwa kipindi cha miezi mitatu.

Akitoa ya taarifa ya utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2024 kwa Vyombo vya Habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Pilly Mwakasege amesema wamefanya ufuatiriaji wa miradi 24 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9.03.

Amesema, miradi 21 kati ya hiyo imeonekana kuwa na mapungufu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.9 kwa kipindi cha ambapo ufatilaji huo ukiwa unalenga kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha iliyotumika kwa (Value For Money).

“Miradi tuliyofuatilia ni ya ujenzi wa miundombinu ya maji,ujenzi wa zahanati,barabara,shule mpya ujenzi wa vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo,bwalo na mabwani katika shule za msingi na sekondari” amesema mwakasege.

Hata hivyo, Mwakasege amewaasa wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuwa waadilifu kwa kuhakikisha fedha zote za zinatumika vizuri na kuongeza juhudi katika usimamizi na kufanya marekebisho ya mapungunfu katika miradi iliyobainika kuwa na mapungufu kwa wakati kama wanavyoshauriwa.

Balozi Kusiluka: Uzoefu utumike kuharakisha mabadiliko
Chama afunguka wanayopitia Msimbazi