Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohamedi Abdallah ‘Baresi’ amesema bado ana imani timu hiyo itasalia Ligi Kuu msimu ujao 2024/25.

Mashujaa FC inashika nafasi ya 13 ikiwa na alama 23 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Singida Fountain Gate Uwanja wa CCM Kirumba, mwishoni mwa juma lililopita.

Baresi amesema bado ana matumaini ya kuibakisha timu hiyo Ligi Kuu pamoja na ukweli kuwa wako kwenye hali mbaya.

“Bado tumebakiwa na mechi kadhaa ambazo naamini tutazitumia vizuri kubaki Ligi Kuu,” amesema kocha huyo wa zamani wa Mlandege ya Zanzibar.

Amesema wanahitaji kuwa mashujaa kuibakisha timu hiyo Ligi Kuu msimu ujao kitu alichosema anaamini kitafanikiwa.

Mei 8 na 11, Mashujaa FC watazikaribisha Young Africans na KMC FC Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na Mei 14 watacheza na Tabora United Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Jurgen Klopp aomba radhi Liverpool
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 25, 2024