Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo, kufuatia kikosi chake kufifisha matumaini matumaini kutwaa ubingwa.

Liverpool walipoteza dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park usiku wa kuamkia leo Alhamis (Aprili 25) kwa kukubali kufungwa 2-0, katika Uwanja wa Goodson Park.

Kichapo hicho kwa Liverpool kilikuwa cha kwanza kwa klabu hiyo ya Anfield dhidi ya Everton tangu 2010.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, ikiachwa alama tatu nyuma ya vinara Arsenal na moja mbele ya Manchester City, ambao wana michezo miwili mkononi.

Alipoulizwa kama Liverpool bado wanaweza kushinda taji hilo ikisalia michezo minne pekee kuchezwa, Klopp ameiambia Sky Sports: “Arsenal na Manchester City lazima wawe na wakati mbaya sana, ili tuweze kufikia malengo ya kuwa mabingwa msimu huu.”

“Sijui. Naweza kuomba radhi kwa mashabiki. Tungefanya vizuri zaidi lakini hatukufanya hivyo na ndiyo maana tukashindwa.” amesema Klopp

MALIMWENGU: Bibi wa miaka 97 apewa talaka kwa kuchepuka
Kocha Mashujaa FC aahidi kubali Ligi Kuu