Johansen Buberwa – Kagera.

Watu wanne wamefariki kwa ajali ya moto na wengine saba kunusurika kifo baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kushika moto  uliotokana na mlipuko wa mafuta ya Petroli, katika Kata ya Rusumo iliyopo Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Akizungumza na Dar24 Media Kamishina msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani humo, Zabrone Muhumhma amesema  tukio hilo limttokea majira ya alfajiri ya leo Aprili 25, 2024 kwenye nyumba hiyo walikuwa wanaishi jumla ya watu 11.

Amesema, nyumba hiyo inamilikiwa na Didas Dominick na kwenye chumba kimoja walikuta miili ya watu wanne waliokuwa tayari wamefariki huku wengine saba wa vyumba vingine wakifanikiwa kutoka salama.

Amewataja waliofariki kuwa ni Rajabu Paulo (16), George Josephat (18) mwingine ametambulika kwa Jina moja la Jastas (22) na Revocatus Jacobo (16) mkazi wa Mubumba Rusumo ambaye alikuwa ni muuzaji wa mayai.

“Uchunguzi unaonesha siku ya jana usiku huyu kijana muuza mayai aliamka na kuchemsha mayai kutokana na kulala usiku walivuta hewa chafu ya ukaa ikawadhuru wakaacha jiko linaendelea kuwaka moto ikasababisha Petroli kulipuka na kusababisha hao kupoteza maisha,” amesema Kamishina Msaidizi Muhumhma.

Mauricio Pochettino azua kizungumkuti Chelsea
Marek Hamsik: SSC Napoli wamekosea mahala