Mahakama Nchini Tunisia, imewahukumu Waandishi wawili wa Habari kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha habari za uongo, zinazodaiwa kuleta taharuki na kutishia usalama wa umma na kufanya jumla ya Waandishi waliofungwa jela kusikia sita.

Akihojiwa na Vyombo mbalimbali vya Habari, Afisa mmoja wa Mahakama aliwataja Waandishi hao kuwa ni Zghidi na Bsaiss, wote wakiwa ni waajiriwa wa Radio ya IFM ambao waliwekwa kizuizini mapema mwezi huu kutokana na maoni ya kisiasa waliyotoa kwenye kipindi chao.

Kwa mujibu wa baadhi ya Waandishi wa Habari, ambao ni Wanachama Chama Kikuu cha Waandishi wa Habari nchini humo, wamesema mbali na hukumu hiyo, pia Waandishi wengine 12 bado wanakabiliwa na mashtaka kama hayo Mahakamani.

 

Sheria mpya za Habari: Tutasubiri mpaka lini? - Wadau
Maadhimisho uhuru wa Vyombo vya Habari: Sauti zimesikika