Mwimbaji nguli wa Nigeria, 2Face Idiba amewaomba Dbanj na aliyekuwa boss wake na mtayarishaji wa nyimbo, Donjazzy kuweka kando tofauti zao na kufanya wimbo mmoja mkali.

2face aliwasilisha ombi lake hilo kwa kiingeza kisicho rasmi (pidgin) wakati wa hafla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akifikisha umri wa miaka 40, hafla iliyohudhuriwa na mastaa wengi wakiwemo Don Jazzy na Dbanj.

Wawili hao walipiga picha ya pamoja katika hali inayoashiria kusahau tofauti zao japo haijafahamika kama wako tayari kufanya kazi pamoja.

CCM Na Chadema Wakwepa Mdahalo Wa Urais, Waishia Tambo
Roma Apokea Ofa Kibao Kushuti Video Ya ‘Viva’