Serikali imesema jumla ya Walimu 9,800 wamepatiwa ajira mpya, na kudai kuwa nafasi 736 za kada za Afya nchini zilizokosa waombaji zinatakiwa kupata waombaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ametoa taarifa hiyo hii leo Juni 26, 2022, wakati akitangaza waliochaguliwa katika ajira hizo zilizotangazwa mapema Aprili, 2022.

Amesema nafasi zilizokosa sifa ni Daktari wa Meno 50, Tabibu Meno 43, Tabibu Msaidizi 244, Mteknolojia Mionzi 86 na Muuguzi ngazi ya cheti 313.

“Upande wa kada ya afya walitakiwa watumishi 7,612 lakini wenye sifa walikuwa ni 6,876 na hivyo kufanya pungufu ya watumishi 736,” amesema Waziri Bashungwa.

Kufuatia hatua hiyo, Serikali imesema kada hizo zinarudiwa kutangazwa tena ili kupata waombaji wenye sifa watakaojaza nafasi zake.

Serikali yamshika mkono aliyefungua mapacha wanne
Serikali 'yawauma sikio' wanaotarajia kupata watoto