Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz amesema Mkutano wa nchi zilizoendelea kiviwanda Duniani G7 unaoanza hii leo Juni 26, 2022, utaangazia suala la mfumuko wa bei za bidhaa, mgogoro kuhusu nishati na tabia nchi.

Scholz ameyasema hayo hii leo na kuongeza kuwa Viongozi wa G7 ambao wataanza mkutano wao wa siku tatu jioni ya leo nchini Ujerumani, watajadili pia athari zinazoukumba Ulimwengu, kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Amesema, kuhimizwa na kuundwa kwa kile alichokiita ‘klabu ya tabia nchi’ kutasaidia Mataifa kufanya kazi pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhusisha siasa za kikanda na urekebishaji wa mizozo ya kudorora kwa chumi.

Hata hivyo, hayo yanatukia huku mamia ya waandamanaji wakijitokeza mjini Munich, wakiwataka Viongozi wa G7 wanaohudhuria mkutano huo wa kilele kuchukua hatua za kumaliza matumizi ya nishati na kupambania suala la njaa ulimwenguni.

Nchi ya Ujerumani inashikilia Urais wa kupokezana wa G7 kwasasa, na pia ni mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika Bavaria.

Serikali 'yawauma sikio' wanaotarajia kupata watoto
Mkandarasi 'abanwa mbavu' mradi wa maji