Beki kutoka nchini Argentina na klabu ya Man City, Martin Demichelis amefunguliwa mashtaka na chama cha soka nchini England FA, kufuatia tuhuma za kujihusisha na michezo ya utabiri (betting).

Beki huyo anatuhumiwa kujihusha na mchezo huo unaopigwa vita duniani, mwezi januari mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na FA imeeleza kwamba “Beki wa Manchester City Martin Demichelis amefunguliwa mashataka kutokana na kwenda kinyume na maadili ya kujihusisha na michezo ya kubahatisha (betting).

Ni kinyume na sheria kwa mchezaji yoyote anaecheza soka nchini England, kujihusha na michezo hiyo kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na FA kupitia kifungu E8.

Demichelis anatuhumiwa kufanya hivyo kati ya Januari 22- 28 mwaka huu.

Amepewa muda mpaka April 5, kuwasilisha utetezi wake kabla ya saa kumi na moja jioni kwa siku hiyo, na kama hautowaridhisha wajumbe wa kamati ya nidhamu ya FA, Demichelis huenda akadhibiwa ama kutozwa faini.

Jerry Muro Alia Na Mlolongo Wa Michezo Inayowakabili
Mwanasiasa Kuwania Nafasi ya Urais ZFA