Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, imewaagiza wakandarasi wa ujenzi wa Barabara zote unaoendelea kufanyika Wilayani humo kuzingatia ubora na kukamilisha kwa wakati.

Maagizo hayo, yametolwewa na Kamati hiyo baada ya kufanyika kwa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), iliyoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, Greyson Mwengu.

Ukaguzi wa ujenzi wa Barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wilayani Muleba, Kagera.

Amesema, katika ziara hiyo kamati ya ulinzi umetembelea Barabara nne ambazo zinajengwa kwa garama ya shilingi bilioni 1.3 nakuongeza kuwa maagizo ya Wilaya ni kuona miradi hiyo inakamilikaa kwa muda uliopangwa na kwa ubora.

Awali, Kaimu Meneja wa Tarura Wilaya ya Muleba alisema, Barabara hizo zinajengwa na wakandarasi wawili tofauti na kwamba pesa za utekelezaji wake zinatoka kwenye mfuko wa Barabara na kwamba utekelezaji wake umefikia asilimia 30 na utababidhiwa rasmi Disemba 2022.

Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, iliyoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, Greyson Mwengu kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara.

Kwa upande wao Wananchi ambao ni watumiaji wa Barabara hizo wameipongeza serikali kwa kuwafungulia barabara ambazo zilikuwa zikiwapa tabu hasa nyakati za masika zilizosababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya upande mmoja na mwingine.

Sudan na Marekani 'zaoneshana tabasamu' baada ya miaka 25
Habari kuu kwenye magazeti ya leo September 2, 2022