Wabunge wapya waliochaguliwa katika Uchaguzi wa Agosti 9 wa Kenya, wamegonga mwamba baada ya juhudi zao za kupata bima inayoshughulikia ukandaji na urembo wao kukataliwa na Tume ya Huduma za Bunge (PSC).

Tume hiyo imesisitiza kuwa upasuaji wa urembo utashughulikiwa tu katika visa vya ajali na gharama zingine ambazo wabunge watajilipia ni pamoja na uchafuzi wa mionzi kutoka kwa mafuta ya nyuklia, taka au milipuko, majanga ya asili na magonjwa yasiyojulikana yanayosambaa eneo kubwa kijiografia bila kuhusisha janga la Covid-19.

Katika nyongeza ya huduma watakazolipia, pia watatumia pesa zao wenyewe kulipia nyumba za wazee, mahali pa kupumzika na matibabu ya mitishamba.

Hata hivyo, wabunge hao watapata bima ya afya ya KSh10 milioni sawa na Milioni 194 na laki tatu za kitanzania ambayo inajumuisha familia zao.

Nation Africa inaripoti kuwa, bima hiyo ya KSh10 milioni sawa na Milioni 194 na laki tatu kwa kila familia pia itatoa huduma ya kulazwa hospitalini kikamilifu na urahisi.

Bunge la Kenya.

Katika bima hiyo mpya, wabunge na wategemezi wao watahitimu kupata bima ya matibabu ya KSh10.65 milioni iwapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea.

Hata hivyo, wabunge watafungiwa nje ya bima hiyo iwapo watapatikana wakihusika katika vitendo vya vurugu au ugaidi.

Mnamo 2021, Wabunge wa Kenya walipendekeza kuanza kupata huduma za ukandaji katika majengo ya bunge katika ripoti iliyowasilishwa na kamati ya Huduma za Vifaa Hitajika Bungeni.

Kamati hiyo ilisema pendekezo hilo ni kwa minajili ya kuimarisha afya ya wabunge kutokana na kukabiliwa na wakati mgumu wanapotunga sheria.

Kamati hiyo iliyokuwa ikioongozwa na Mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu ilisema kituo hicho pia kinatakiwa kipanuliwe ili kuongeza vyumba vya ukandaji, kinyozi na ususi.

Mashabiki waombwa kuiunga mkono Taifa Stars
Zoran Maki: Michezo ya Sudan imetuimarisha