Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania – TACAIDS, yaliyolenga kuufahamu muundo na utendaji wa Tume, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake kukutana na Idara na Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania alipokutana nao mapema Machi 10, 2023 Jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Machi 10, 2023 Jijini Dodoma, Dkt. Yonazi  ameipongeza Tume kwa kazi nzuri wanazofanya na kueleza ni muhimu kuongeza kasi zaidi katika kuyafikia malengo na kuhakikisha jamii inapata huduma na elimu kadiri iwezekanavyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akieleza kuhusu muunda wa Tume wakati wa kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi alipokutana na timu ya menejimenti ya Tume Jijini Dodoma Machi 10, 2023.

Amesema, “Ninawapongeza TACAIDS kuendelea kusaidia katika mapambano haya na kila jitihada zinazofaywa zina tija katika kuyafikia malengo hivyo, tuendelee kutoa elimu kwa umma kwa kuzingatia kuwa mnayagusa maisha watu.”

Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TACAIDS Yasin Abbas akichangia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu alipokutana na menejimenti ya Tume hiyo Jijini Dodoma.

Aidha, ameongezea kuwa Ofisi yake ipo wazi na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tume hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli zinazotekeleza na Tume.

Walioathirika na mimba za utotoni wasitengwe
Serikali kuimarisha mazingira wezeshi kibiashara: Dkt. Mwinyi