Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho amesema yupo tayari kuzungumza na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic, ili akubalia kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Mourinho ametoa ahadi ya kuzungumza na mshambuliaji huyo, mbele ya waandishi wa habari katika mkutano maalum ambao ulikua unazungumzia mchezo wa ligi kati ya Man Utd dhidi ya Southampton utakaochezwa hii leo katika uwanja wa Old Trafford.

Mourinho alisema anatambua mshambuliaji huyo ana malengo tofauti, na ndio maana alikubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Man Utd, lakini akasisitiza kufanya jitihada za kumshawishi.

Alisema anaamini suala hilo litawezekana kutokana na ukaribu uliopo kati yake na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye tayari ameshaifungia Man Utd bao moja katika ligi ya England, utasaidia mpango huo kufanikiwa kama anavyotarajia.

“Ninamuona ni mtu mwenye furaha tangu alipokuja hapa, naamini atakubakli kuendelea kuwa na Man Utd kwa mwaka mwingine mmoja,” alisema Mourinho.

Ibrahimovic alijiunga na Man Utd kama mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) mwishoni mwa msimu uliopita.

Lema afunguka uteuzi wa Mkuu wa Mkoa Mpya Arusha, "Nilijua..."
Danny Welbeck Kurejea Uwanjani Mwishoni Mwa Mwaka