Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa kama vyama vya upinzani vinania ya kuing’oa CCM ni vema vikaungana kwa dhati.
Ameyasema hayo kisiwani Pemba, Wilaya ya Chakechake katika ziara ya Chama hicho ya kutembelea majimbo Chama hicho katika kisiwa hicho.
Amesema kuwa Watanzania wamechoshwa na utawala uliopo madarakani na wanataka mabadiliko lakini tatizo vyama vya upinzani vimbetwanyika na kuzigawa kura kwa CCM.
“Tusijidanganye umoja ndio silaha pekee ya kuing’oa CCM Tanzania bila ya umoja hatutafanikiwa,”amesema Maalim Seif.
Aidha, amesema kuwa anaamini kuwa ipo siku atakuwa rais wa Zanzibar na kuongeza kuwa siku si nyingi haki yake ya kuwa rais ataipata.
Hata hivyo, Maalim amekituhumu Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumtumia Prof. Ibrahim Lipumba kwa kutaka kukivuruga Chama Chama Wananchi CUF, na kwamba hawatafanikiwa.