Mcheza kikapu wa klabu ya Beijing Ducks ya nchini China, Stephon Marbury, amemnanga gwiji wa mchezo huo Michael Jordan kwa kumtaja kama mwizi wa mchana katika bidhaa zake za kibishara.

Marbury, ambaye ni raia wa nchini Marekani, amediriki kufiklia hatua ya kunanga hadharani, Michael Jordan kutokana na kuchukizwa na kujikwaza katika bidhaa zake ambazo zinaonekana kuwa na thamani ya juu.

Marbury, amesema Jordan amekua hawatendei haki mashabiki pamoja na watu wa kawaida ambao wanapenda kununua bidhaa zake hususan viatu vya Air Jordan, kwa kuviweka sokoni kwa gharama ya dola za kimarekani kuanzia 70 hadi 220.

Amesema haoni sababu ya mtu huyo kufanya hivyo, kutokana na ukweli wa bidhaa zake anazoziweka sokoni kutengenezwa kwa gharama ya dola 5 kwa kiatu kimoja.

Marbury mwenye umri wa miaka 38, amefikia hatua ya kubwatuka na kuuelezwa umma wa mashabiki wa Michael Jordan namna wanavyoibiwa, kutokana na yeye mwenyewe kuwa na bidhaa ya viatu ambavyo ipo sokoni kwa sasa vyenye nembo ya Marbury’s footwear.

Kikatu cha Marbury’s footwear kinauzwa kwa dola za kimarekani 15.

Michael Jordan amekua akitengeneza viatu vyake kwenye kiwanda kimoja na Stephon Marbury na gharama wanazotozwa ni sawa kutokana na ubora wa bidhaa zao kufanana.

Umoja Wa Mataifa Waelezea Picha Ya Ushindi Uchaguzi Mkuu
Watendaji Wa Tanesco Kufutwa Kazi Na Rais Huyu Wa Awamu Ya Tano