Serikali imelifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa muda wa miaka miwili kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abassi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa serikali imechukua uamuzi wa kulifumgia Gazeti hilo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017, ambapo amesema kuwa kwa muda mrefu  idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

“Tulipowaita wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa habari lazima izingatie maadili,” amesema Dkt. Abbas

Aidha, Dkt. Abbas amezitaja baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari “Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM”. na kusema kuwa habari hiyo ilikuwa na lengo la kuichafua ofisi ya Rais, nyingine aliyoitaja ni makala iliyoandikwa jana katika gazeti hilo yenye matusi, dhihaka na maneno yasiyofaa dhidi ya Rais John Magufuli

Sentensi 4 tata zilizomkera Zari wa Diamond
Mlinda mlango Goran Lenac apigwa risasi