Mshambuliaji mpya wa Azam FC Abdul Seleman Sopu amefunguka kwa mara ya kwanza namna alivyozitosa klabu nguli katika Soka la Bongo Simba SC na Young Africans.

Sopu alisajiliwa Azam FC saa kadhaa baada ya kufanya maajabu makubwa kwenye mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kwa kufunga mabao matatu pekee yake dhidi ya Young Africans, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Coastal Union amesema ni kweli Simba SC na Young Africans zilikua na mpango wa kumsajili katika kipindi hiki, lakini alionyesha msimamo wa kuthamini uwezo wake kwa kuangalia Maisha yake ya ndani ya Uwanja.

Amesema hakushindwa kuchagua moja ya vilabu hivyo, lakini aliamini katika kucheza soka lake kila kukicha akiwa kwenye kikosi cha kwanza, na mahala sahihi aliona ni Azam FC ambayo imekua ikithamini vijana na kuwapa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Simba SC na Young Africans ni timu kubwa, lakini Azam FC ni kubwa pia. Niliziona ofa zao ila niliamua kwenda Azam FC nikiamini ndio sehemu sahihi zaidi ya kucheza muda huu”

“Haikuwa rahisi kwani wengi walitamani niende kule lakini binafsi nilifuata matakwa yangu na Azam FC ilinipa ushirikiano wa kutosha hadi naenda kusaini kila kitu kilikuwa tayari”

“Dhumuni langu ni kuendelea kucheza mara kwa mara kama nilivyokua Coastal Union, naamini Azam FC nafasi hiyo nitaipata na kuendelea kuonyesha uwezo wangu, soka ni mchezo wa wazi ninaamini kila hatua yangu itaonekana katika klabu hii.” Amesema Sopu

Nasreddine Nabi achimba mkwara Young Africans
Tanzania kuwa kitovu biashara ya Madini