Mshambuliaji kutoka nchini Sweden na klabu Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kupokea ofa za baadhi ya klabu za zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka Ufaransa mwishoni mwa msimu baada ya mkataba wake na matajiri hao wa jijini Paris utakapomalizika na mbio za kuwania saini yake zimeanza.

Klabu tatu za jijini London Arsenal, Chelsea na West Ham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, lakini Zlatan amesisitiza kufanya maamuzi mara atakapotulia na kufikiria ni wapi patakapomfaa kucheza soka leke.

Akizungumza kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Sweden na Jamhuri ya Czech, Ibrahimovic amesema: “Ndiyo, kuna timu zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini England zinitaka, naweza kuthibitisha hilo.

“Ligi kuu ya soka nchini England, ni maarufu sana duniani na kila shabiki anaizungumzia. Mambo mengi inabidi uyafikirie vizuri wakati nitakapofanya maamuzi mwishoni mwa msimu,”

“Wakati utakapofika, wakati kete zipo mezani, hapo ndipo nitakapoamua wapi pa kwenda kutokana na kipi ninachotaka ndipo tutaona zaidi,”

“Ni kama ndoa. Pande mbili zinatakiwa kuihitaji, siyo tu mmoja au mwingine. Kila upande unatakiwa kuitaka kama upande mwingine,” amesema.

Babu Wa Young Africans Aanza Kuvuta Harufu Ya Ugumu Wa Al Ahly
Super D: Tujenge MGM Grand Garden Arena Ya Tanzania